Red Cross Society Katavi

From OpenStreetMap Wiki
Jump to navigation Jump to search

Taarifa za awali

Barua pepe

trcs.katavi@trcs.or.tz

Jina kamili la muombaji

Sheby Mloti

Una akaunti ya OSM?

Ndio

Ikiwa ndio taja jina lako la matumizi ya OSM kama hakuna andika N/A

Sheby Mloti

Tafadhali taja majina kamili na majina ya akaunti ya OSM ya mtu yeyote wa ziada atakayeongoza utekelezaji wa mradi ikiwa programu hii itafanikiwa

Agness kayegele na Songambele Otaru

Ikiwa una akaunti ya OSM Tafadhali tiki kwenye visanduku hali yako ya uchanguaji

Mgeni katika uchangiaji

Taja jina la kikundi cha jamii / shirika linawasilishwa kwa niaba ya katika maombi haya

Red cross society katavi

Je! Shirika lako / kikundi cha jamii kimesajiliwa kisheria?

Ndio

Ikiwa umeonyesha hapana hapo juu, tafadhali andika jina la shirika ambalo litaweza kupokea pesa za udhamini kwa niaba yako.

N/A

Taja Pendekezo la eneo la mradi utakapofanyika

Wilaya ya Tanganyika kwenye vijiji vya karema na ikola na itetemya

Je! Hapo awali ulishapewa ufadhili wowote wa mradi ?

Hapana

Tafadhali onyesha jumla ya kiwango cha pesa unayoomba kwa TSH

8,800,000 Tshs

Taarifa Kuhusu Mradi

Je! Ni shida gani ambayo utafanyia kazia au kushughulikia ili kuitatua katika jamii yako?

(Katika sehemu hii tafadhali fafanua kwa kina changamoto ambayo mradi wako unashughulikia.Tunapendekeza jibu lako liwe na kiwango cha chini cha maneno 100 na yasizidi maneno 300.)

Vijiji vya Karema , ikola na itetemya vinapakana na Nchi ya Jamhuri ya Congo na vijiji hivi vina changamoto kubwa ya muingiliano wa watu toka Nchi ya Congo na Burundi na hasa watu kuingia kwa kupicha kwenye mipaka isiyo rasmi(entry points) na kutokana na changamoto za magonjwa ya milipuko na maafa kumepelekea vijiji hivi kuwa sehemu hatarishi na vyanzo vikubwa vya maradhi kama ebola na corona.Kwahiyo bila ys kuweka kwenye ramani mipaka yote bubu na nkia zote za panya zikajulikana ili Red cross navwadau wengine wakaweza kuweka huduma za afya na kijamii.Vijiji hivi vinawezakuwa hatari sana kwa maisha ya watanzania na wageni pia

Ni nini kinachokuchochea kufanyia kazi suala hili?

(ni nini sababu iliyosababisha, imekuhimiza ufanye kazi juu ya suala hili, Tunapendekeza jibu lako liwe na kiwango cha chini cha maneno 100 na yasizidi maneno 300.)

Tumeshuhudia wageni wengi kutoka Nchi jirani wakija na baadaye kutambulika kuwa wamekuja na magonjwa mbalimbali kama ebola na corona.pili kumeshawahi kutokea mafuriko katika vijiji hivi kwahiyo maeneo husika yanatakiwa kuwekwa kwenye ramani na kuhasisha watu kuhamisha makazi yao na tatu kuna uhitaji mkubwa wa kuwekwa kwenye ramani huduma zote za kijamii na kiseikali vijiji hivi ili iwe rahisi wakati wa utekelezaji endapo maafa au majanga yatatokea tena

Umewahi kufanya kazi kutatua shida hiyo hapo awali?

Ndio

Ikiwa ndio Umefanya nini tayari kutatua suala hili?

(Tafadhali eleza na onyesha mafanikio yako makubwa, Tunapendekeza jibu lako liwe na kiwango cha chini cha maneno 100 na yasizidi maneno 300.) Ikiwa hakuna, andika N / A

Tumehamasisha na kutoa elimu kwa wanavijiji kuhusu utayari na kujikinga na madhara ya maafa na majanga na magonjwa ya mlipuko

Ikiwa ndio Ni changamoto zipi ulizokabiliana nazo katika kazi yako ya kutatua suala hili, na ulitatua vipi changamoto hizo?

(Tafadhali bainisha na onyesha changamoto zako kubwa ulizokumbana nazo na ulizitatua vipi, Tunapendekeza jibu lako liwe na kiwango cha chini cha maneno 100 na yasizidi maneno 300.) Ikiwa hakuna, andika N / A

Vijiji vyote havipo kwenye ramani kwahiyo ni ngumu kujua huduma zipo wapi na matatizo yapo wapi.pili ni ukosefu na upingufu wa rasilimali fedha

Ikiwa hapana, unatarajia changamoto gani wakati unafanya kazi ya kutatua suala hilo?

(Tafadhali bainisha na onyesha changamoto unazo his utakumbana nzo kaika utekerezaji wa mradi huu. Tunapendekeza jibu lako liwe na kiwango cha chini cha maneno 100 na

yasizidi maneno 300.) Ikiwa hakuna, andika N / A

N/A

Eleza ni upi mpango wako endelevu

(Katika sehemu hii tafadhali fafanua jinsi shughuli zako zitaendelea baada ya ufadhili. Ikiwa unaomba ufadhili wa kununua vifaa, eleza ni nani atakayehifadhi / kutumia vifaa unavyonunua, na kama una mipango endelevu wa maendeleo ya jamii yako. Tunapendekeza jibu lako liwe na kiwango cha chini cha maneno 100 na yasizidi maneno 300.)

Vifaa vitakuwa chini ya uangalizi wa Red cross tawi la katavi.Na volunteers na members watafundishwa na kuhasishwa jinsi ya kutumia open data source na mapping activities.Kazi ya kumapp itaendelea sehemu na miradi mbalimvali ya Red cross na wadau wengine

Lengo la Mradi

Je! Mradi huu una malengo gani katika jamii?

(Tafadhali elezea malengo ya mradi. Hii inaweza kujumuisha: kuweka malengo kama "tutafundisha idadi ya X ya jamii mpya," tutasajili kama taasisi ya kisheria ", au" data itatumiwa na X ", na kwanini malengo haya ni muhimu kwa jamii yako kama vile "tunakusudia kushirikisha idadi ya X ya wanawake katika shughuli za kuchora ramani ili tuweze kuwawezesha wanawake wa eneo hili" Tunapendekeza jibu lako liwe na kiwango cha chini cha maneno 150 na yasizidi maneno 300.)

Tutafundisha members wetu wa Red cross jinsi ya kutumia open data source na mapping activities

2.Tutakuwa tunatumia data na information tutakazozikusanya katika kusaidia kubadirisha maisha ya walenga

3Tutaongea mapping activities katika Mkoa wa Katavi

Je! Malengo ya muda mrefu ya mradi ni yapi?

(Tafadhali eleza maono ya mradi wako. Hii inaweza kujumuisha: ambapo unaweza kuona mradi wako kwa muda wa miaka mitano, jinsi unataka data yako itumiwe, ushirikiano wa baadaye ambao ungetaka kuanzisha, au jinsi ungependa mradi wako ukue apo baadae Tunapendekeza jibu lako liwe na kiwango cha chini cha maneno 100 na yasizidi maneno 300)

Baada ya kuwafundisha wengi kujua na kupenda open data na shughuri za kumapp tungependa kuendelea na miradi mingine kama ya kuweka kwenye ramani vijiji vinavyoathiriwa na migogoro ya tembo na binadamu kule mbuga ya Katavi na kushirikiana na wahusika katika kutatua matatizo yaliyopo

Orodhesha zana/vifaa unavyotarajia kutumia wakati wa mradi wako na kwanini

(Tafadhali eleza ni zana/vifaa zipi unapanga kutumia kukusanya, kusasisha, kusafisha, au kuhifadhi data na kwanini. Tunapendekeza jibu lako liwe na kiwango cha chini cha maneno 100 na yasizidi maneno 300.)

Maps me, kobobox tools(Odk) na OSMAnnd

Je! Unahitaji maarifa au ujuzi gani wa ziada ili kuboresha ufanisi wa mradi?

(ikiwa kuna mafunzo yoyote ya kuongeza utahitaji mfano jinsi ya kutumia zana za chanzo wazi, jinsi ya kuandika ripoti nzuri nk tafadhali elezea hapa chini na kwanini, Tunapendekeza jibu lako liwe na kiwango cha chini cha maneno 100 nayasizidi maneno 300) Ikiwa hauna andika N/A

N/A

Eleza jinsi unavyopanga kusambaza ujumbe wako/mafanikio ya mradi kwa jamii

(Tafadhali toa mifano njia utatumia kuambaza ujumbe wako kwa wengine. Hii inaweza kujumuisha: jinsi utakavyotangaza habari yako, wapi utaonesha yaliyomo kwenye vyombo vya habari , jinsi utatumia njia za mitandao ya kijamii,. Tunapendekeza jibu lako liwe na kiwango cha chini cha maneno 100 na yasizidi maneno 300.)

Tutatumia mitandao yote ya kijamii ya Red cross na wadau wengine na pia tutatumia radio zetu za jamii za hapa Mpanda na kutuma maandiko kwenye magazeti yetu na mikutano ys kila mwezi na wadau

Umilikishwaji

Eleza ni nani atakayemiliki / kupata/kunufaika na kutumia data au mafunzo yatokanayo na mradi huu

(Ni muhimu kwamba data unayotengeneza wakati wa mradi iwe na matumizi , na kwamba itatumika kutatuta changamoto za kibinadamu au za kimaendeleo katika jamii. Katika sehemu hii, tafadhali jumuisha: ikiwa data utakayokusanya imeombwa na nani, ikiwa kuna uhusiano rasmi na shirika lolote, na ikiwa kuna MoU iliyopo kati yako na shirika unaloloshirikiana, na kwa muda gani umekuwa ukifanya kazi na shirika unaloshirikiana nalo. Ikiwa shirika lako au jamii itakuwa mtumiaji wa data, tafadhali fafanua jinsi watakavyotumia data hiyo, na watafikiaje/wataipataje data pia kuna uwezekano wa mashirika mengine yanayofanana kupata na kumiliki data hiyo?. Tunapendekeza jibu lako liwe na kiwango cha chini cha maneno 100 na yasizidi maneno 400.)

Data zitakuwa zinatumika na Red Cross na NGOs zote na Serikali ya Mkoa na hasa idara ya elimu na afya

Eleza kama kuna jamii / shirika lingine lolote unalopanga kulikaribia na kushirikiana ili kuwapatia data kwa madhumuni ya kukuza lengo la mradi

(Katika sehemu hii, tafadhali fafanua washirika wowote wa ziada ambao unaweza kuwakaribia au kushiriki data nao kwani wameonyesha hitaji la data itakayokusanywa. Ikiwa hakuna washirika wa ziada (zaidi ya mtumiaji wa data) hii lazima isemwe hapa. Tunapendekeza jibu lako liwe na kiwango cha chini cha maneno 100 na yasizidi maneno 300.) ikiwa

hakuna andika N / A

Jeshi la zima moto na Katibu wa afya Mkoa wanahitaji hizi data kwa matumizi yao ya sasa na baadaye

Ujumuishwaji

Utahakikishaje kuwa shughuli zako za mradi zitazingatia jinsia au watoto?

(Tafadhali eleza jinsi utakavyoshirikisha wanawake / wasichana au watoto wa shule katika shughuli zako za mradi. Tafadhali ingiza idadi ya wanawake, wasichana au vikundi vilivyotengwa unavyopanga kufanya nao kazi , na wakati gani katika shughuli zako unapanga kuwashirikisha. Tunapendekeza jibu lako liwe na kiwango cha chini cha maneno 100 na yasizidi maneno 300).

Mradi utazingatia jinsia na hasa katika kufundisha na kuhamasisha utumiaji na usomaji wa open data source na mapping activities. Wasichana wengi watashirikishwa

Mapinduzi ya ujuzi huria

Eleza jinsi unavyopanga kupanua jamii yako kwenye swala zima la matumizi/utengenezaji wa ramani/data

(Katika sehemu hii, tafadhali ainisha : njia yako utakayotumia kufanya kazi katika eneo la pembezoni mwa tanzania ili kupanua maarifa, utashirikishaje na jamii mpya kutoka kwa jamii isiyojulikana, idadi ipi ya watu wapya unaopanga kufanya nao kazi , na unampango gani ili uweze kudumu nao muda wote wa mradi na zaidi. Tunapendekeza jibu lako liwe na kiwango cha chini cha maneno 100 na yasizidi maneno 300.)

Tutafundisha kwenye mashule na vyuo na hasa chuo cha Veta na cha Nursing

Ushirikiano

Eleza jamii ambazo tayari unafanya kazi nazo

(Hii inaweza kujumuisha serikali za mitaa, sekta binafsi, taasisi au jamii za OSM (kama mifano). Ikiwa haujafanya kazi na jamii yoyote hapo juu, tafadhali sema hilo na ueleze jinsi unavyopanga kufanya kazi na jamii zingine katika mradi wako).Tunapendekeza jibu lako liwe na kiwango cha chini cha maneno 100 na yasizidi maneno 300.)

Tunafanya kazi na Serikali ya Mkoa na hasa kwenye idara ya afya , elimu na mendeleo.Tunashirikiana pia na NGOs mbalimbali hapa mkoani

Eleza jamii zingine unazopanga kuwasiliana nazo, au kuanzisha uhusiano na, kwa madhumuni ya mradi huo

(Tunapendekeza jibu lako liwe na kiwango cha chini cha maneno 100 na yasizidi maneno 300.)

Makundi mbalimbali ya mapaphons na Jeshi la zima moto

Viambatanishi

Tafadhali amabatanisha toleo la PDF la bajeti yako uliyopendekeza

(Bajeti yako lazima iwe ya kina na ya kweli. Mahesabu yanapaswa kuwa sahihi, na matumizi ya bajeti yanapaswa kuakisi na shughuli zilizoelezewa katika mpango wa mradi. Lazima utoe maelezo kwa nini unahitaji kitu unachotengenezea bajeti. Kwa kutumia mfano huu wa bajeti. https://docs.google.com/document/d/1sGPkshy6uZGlqtJHw1ipdplw9LmLUFvDF1B3RFAAU edit?usp=sharing. Hakikisha unaandika jina la mradi kama jina la PDF ukayotuma)

Link ya bajeti

Tafadhali ambatanisha toleo la PDF la mpango wako wa mradi uliyopendekeza

(Mpango wa mradi lazima uwe wa kweli, na lazima utoe ratiba ya kina ya shughuli zilizoainishwa katika programu yako. Tunapendekeza kwamba ueleze shughuli zako kwa ufupi na uoanishe kwa wazishughuli hizo kwa kulingana na maelezo ya bajeti yako. Kwa kutumia mfano huu wa mpango kazi

https://docs.google.com/spreadsheets/d/1rLcERRARB2slRrgySPTmj_kWexV3d3IhPWSJsCBUlyg/edit ? usp=sharing Hakikisha unaandika jina la mradi kama jina la PDF ukayotuma)

Link ya mpango kazi

Uwasilishwaji

ikiwa inafaa, tafadhali weka link ya tovuti ya shirika lako Ikiwa hakuna, andika N / A

N/A

Ikiwezekana, tafadhali weka link ya akaunti ya facebook ya shirika lako Ikiwa hakuna, andika N / A

N/A

Ikiwezekana, tafadhali weka link ya akaunti ya twitter ya shirika lako Ikiwa hakuna, andika N / A

N/A

Je! ufadhili huu utafadhili mradi uliowekwa/unaofanyika tayari?

Hapana

Tafadhali thibitisha kuwa umekagua maombi yako, na umejibu maswali kwa kadiri ya uwezo wako

Ndio - ningependa kuwasilisha ombi langu